KARIBU MKURANGA

Tuesday, July 17, 2012

 TUIJENGE MKURANGA YA KESHO, WAKATI NI HUU

Ndg zangu tuna kazi kubwa ya kutimiza ndoto, njozi na hamasa yetu kutimia. Miezi michache imebaki kwa Ndg zetu kidato cha nne kuanza mitihani ya taifa na programu yetu ya kufundisha inasusua kwa kukosa fedha za kuerejesha nauli kwa wanaojitolea kufundisha na kuwapa hamasa ndogo.

HALI IKOJE?
Mkoa wa Pwani ni wa pili toka mwisho baada ya Shinyanga kwa viwango vibovu vya ufaulu na Mkuranga ni ya mwisho kimkoa. Mkuranga Ndio Kwetu, hatuwezi ikimbia aibu hii, hatuwezi kuwa na fahari ya kwetu ikiwa tunazalisha sifuri kwa wingi kimkoa na kitaifa

NINI CHA KUFANYA?
Ili tujipambanue tuko tofauti na wengine na tudhibitishe kweli tuna nia, uchungu na mapenzi ya dhati na Mkuranga basi tutimize wajibu wetu na ahadi zetu.

KIVIPI
1. Wale tulio mbali na Mkuranga na tunao uwezo wa kuchangia kile kima angalau 20,000/= kwa mwezi tufanye hivyo. Allah atufanyie wepesi Inshallah kwa kutoa na wenye uwezi zaidi tuchangie zaidi, Kwa niaba yenu nimemshukuru kaka yetu Abdallah Ulega amehaidi kuchangia Million moja mwisho wa mwezi huu

2. Wale waliomaliza kidato cha sita, vyuo pamoja na wale walioko vyuoni na hata makazini kama una likizo na nafasi inapatikana tujitoe kidhati kwa sasa katika kipindi hiki cha lala salama kulikoni kusubir aibu itufike tena na tuanze kumtafuta mchawi wetu.

3. Wenye kuweza kupata nyenzo na vifaa vya kufundishia, kujifunzia au kwa namna yeyote inaweza rahisisha zoezi hili wakati ndio huu

MICHANGO INAKUSANYWA NA NANI?
Bado michango inakusanywa na dada/mama/shangazi yetu Mh Farida Mgomi, kwa niaba yenu nilimshukuru pia kwa kuendelea kukubali jukumu hili hata baada ya kupewa majukumu makubwa ya kitaifa. Tunaweza tuma kwa M-Pesa na Tigo Pesa kwa no zake 0715 371919 au 0757 371919.

NANI ANARATIBU ZOEZI LA KUFUNDISHA?
Kwa wale Allah atawapatia wakati wa kujitolea kudundisha mnaweza wasiliana na katibu wa sekretariat yetu Nyimgeni Mohamedi ndio anaratibu zoezi hili zima. Shukrani kwake na timu nzima inayoendela kupambana kwa niaba yetu japo kwa mazingira magumu na tunawaacha wapweke kana kwamba ni programu yao pekee.

Tuwasiliane kwa maswali zaidi,

Baraka Mwago,
Kaimu M/kiti wa jumuiya hii,
0713/787 094 824
barakamwago@yahoo.com
www.mkurangandiokwetu.blogspot.com


Thursday, June 28, 2012

MKURANGA KUTEMBELEWA NA TUME YA MAREKEBISHO YA KATIBA, WADAU TUJITOKEZE.

Tume ya Marekebisho ya katiba nchini iliyo chini ya M/kiti wa Jaji mstaafu na waziri mkuu  mstaafu wa Tanzania Joseph Warioba watakuwa wilayani Mkuranga kwa siku 4 na vituo 8 tofauti kwa saa na tarehe zifuatazo:-

1. Mkuranga mjini 10/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
2. Vikindu tarehe 10/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
3. Kisiju tarehe 11/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
4. Magawa 11/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
5. Panzuo tarehe 12/07/2012 kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
6. Kimanzichana 12/07/2012 kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni
7. Shungubweni 13/07/2012  kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 6:00 mchana
8. Nyamato 13/07/2012  kuanzia saa 8:00 mchana mpaka 11:00 jioni

Shime shime wana Mkuranga hususani wenye mwamko mkubwa tujitokeze tukaseme na kutoa maoni yetu katika katiba mpya, tuseme tunadhani nini sahihi, nini kiwepo na nini kisiwepo.

Mkuranga itajengwa na wana mkuranga, tuwakilishe vyema wilaya yetu, wajumbe wakitoka kwetu wakiri kuwa kweli walikutana na watu makini na sio vilaza, wapate taswira halisi ya watu wa Mkuranga hususani kizazi chetu chenye mwamko na hamasa kubwa.

Wasalaam,
M/Kiti wenu

Friday, June 22, 2012

KIKAO CHA KESHO WADAU WA MKURANGA NDIO KWETU CHA HAIRISHWA

Assalam Alyekum,
Nawausia na kuisia nafsi yangu tuwe wacha mungu na Allah atufanyie wepesi tuwesze kupata fursa ya kusali Salat -Jumaa.

Nachukua fursa hii kuwajuza wadau wote wa maendeleo ya Mkuranga kupitia jukwaa hili letu la vijana wasomi toka Mkuranga kikao cha kesho tarehe 23/06/2012 kimeharishwa mpaka tutakapojuzana.

Sababu za kuhairisha
1. Wajumbe/wadau wachache pekee ndio waliothibitisha kuhudhuria
2. Kuwapa fursa ndg zetu ambao bado wanafanya mitihani vyuoni kumaliza kwa wepesi.

Kwa taarifa hii tunaomba kupokea maoni yenu ni wakati gani muafaka wa kikao hiki kifanyike? wapi? lini na saa ngapi?

Wabillah Tawfiq,

Baraka Mwago
Kaimu M/kiti wa jumuiya

Sunday, June 10, 2012

WANA JUMUIYA YA MKURANGA NDIO KWETU WALIOCHUKUA FOMU WAREJESHA FOMU ZAO


Habari zilizopatikana na kudhibitishwa na wadau wenyewe ni kuwa ndugu, jamaa na rafiki zetu Ndg Nyimgeni Mohamed, Ndg Juma Nguvumali na Iddi Majuto wote wamerejesha fomu za kuomba ridhaa ya chama cha mapinduzi kuongoza jumuiya ya vijana ya chama hicho kupitia ngazi ya wilaya.
 Kila la kheri kina waukae, mkuranga inawahitaji leo kuliko wakati mwingine wowote, rai yangu kwenu kwa wale ambao kura hazitatosha msikate tamaa bado mnaweza kupata fursa ya kuwatumikia wana Mkuranga kwa nyanja zingine na kwa fursa nyingine.

Wassallam,
Baraka Mwago,
Kaimu M/kiti 
Mkuranga Ndio Kwetu

KENYA YAPATA MSIBA WA WAZIRI WA USALAMA WA NDANI

           Marehemu Prof. George Saitoti enzi za uhai wake
 
Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijabainika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.

Miili ya marehemu imeungua vibaya na moto hivyo utambuzi wa miili hiyo utakuwa mgumu.Mkuu wa polisi aelekea eneo la tukio.Chanzo cha ajali hiyo mbaya bado hakijajulikana.Tetesi zimeshaanza kuhusisha ajali hii na kikundi cha ugaidi cha Al Shabab cha nchini Somalia pamoja na mbio za urais nchini Kenya.RI.P marehemu wote.
You might also like:


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO YAPATA PIGO, MZEE MAKANI AFARIKI DUNIA


BOB MAKNI KADA NA MUASISI  WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA AFARIKI. BOB MAKANI ALIKUA MWENYEKITI WA CHADEMA KABLA YA MBOWE. PIA BOB MAKANI ALISHAKUWA MSAIDIZI WA GAVANA BENKI KUU YA TANZANIA. MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI.
 HISTORIA YAKE CDM-Katibu Makuu wa kwanza wa CHADEMA kati ya mwaka 1993 hadi 1998, Mwenyekiti wa CHADEMA kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 na mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kati ya mwaka 1995.

Saturday, June 9, 2012



TUIFAHAMU MKURANGA YETU VYEMA


Mkuranga is one of the 6 districts of the Pwani Region of Tanzania. It is bordered to the north by Dar es Salaam, to the east by the Indian Ocean, to the south by the Rufiji District, and to the east by the Kisarawe District.
According to the 2002 Tanzania National Census, the population of the Mkuranga District was 187,428.
 
The people of Mkuranga primarily belong to four ethnic groups — the Zaramo, Ndengereko, Matumbi and Makonde. Most people live in poor and simple houses thatched by grass or coconut leaves, poles, and mud walls on earth floors. Fuel wood is the major source of energy for cooking. The Mkuranga District has two government health centers, fifteen government and ten private dispensaries. Traditional health care systems that operate in the district include traditional healers.
 
1. Population and Household Size in Mkuranga Ward
Type
Population (Number)
Household
Male
Female
Total
Number
Average Size
Mkuranga
Mixed
12,741
13,810
26,551
6,083
4.4
Tambani
Rural
7,302
7,438
14,740
3,578
4.1
Vikindu
Mixed
10,938
11,134
22,072
5,322
4.1
Mbezi
Rural
4,249
4,403
8,652
2,040
4.2
Shungubweni
Rural
1,367
1,381
2,748
590
4.7
Kisiju
Rural
6,935
6,897
13,832
3,138
4.4
Magawa
Rural
3,988
4,069
8,057
1,967
4.1
Kitomondo
Rural
5,710
6,095
11,805
2,695
4.4
Lukanga
Rural
6,184
6,473
12,657
2,768
4.6
Nyamato
Rural
6,013
6,186
12,199
2,652
4.6
Kimanzichana
Mixed
8,037
8,927
16,964
3,698
4.6
Mkamba
Mixed
7,076
7,444
14,520
3,050
4.8
Panzuo
Rural
2,980
2,647
5,627
1,343
4.2
Bupu
Rural
2,866
2,691
5,557
1,346
4.1
Mwalusembe
Mixed
5,328
6,119
11,447
2,667
4.3
District Total
91,714
95,714
187,428
42,937
4.4